Zimebaki siku tisa tu mpaka kuifikia October 25 2015 siku ya uchaguzi mkuu Tanzania ambao upo kwenye headlines na CCM, UKAWA na ACT WAZALENDO pamoja na vyama vingine vinavyoshiriki.
Post hii ni maalum kukukutanisha na
matukio ya Mwanza na Mbeya ambako CCM na UKAWA wamehusika ambapo kwa
Mwanza, ni mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa alivyokua akisubiriwa
nje ya hoteli aliyofikia, watu walikua wakikaa nje kwa saa kadhaa ili
kumuona, unaweza kusikiliza ilivyokuwa kupitia hii sauti hapa chini.
Kwa upande wa CCM Mbeya, Katibu wake mkuu Abdulrahman Kinana aliongea na Wananchi na nina mnukuu akisema ‘Sisemi
kwamba CCM hatujafanya makosa, tumefanya makosa na tumekuwa na kasoro
pamoja na mapungufu lakini nani asie na mapungufu? tumejitahidi wengine
walaji wengine waporaji, wengine hawasaidii Wananchi, wengine uongozi
kwa maslahi yao… haya ni mambo tunahangaika kubadilisha kila siku‘
Ukitaka kumsikiliza zaidi Katibu mkuu Abdulrahman Kinana na Wafuasi wa Edward Lowassa unaweza kubonyeza play hapa chini….

Note: Only a member of this blog may post a comment.