Thursday, October 29, 2015

Anonymous

Breaking News: Dr MAGUFULI Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania! MATOKEO Yote Jumla Haya Hapa

Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili wiki iliyopita.

Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr Magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%

Dr Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.