Ikiwa zimepita zaidi ya siku kadhaa toka klabu ya Liverpool ya Uingereza imfukuze kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers, kulikuwa na stori za makocha kadhaa kurithi nafasi hiyo kabla ya Alhamisi ya October 8 uongozi wa klabu hiyo ulithibitisha kuwa kocha mpya wa klabu hiyo ni Jurgen Klopp.
Jurgen Klopp amethibitishwa kujiunga na klabu ya Liverpool kama kocha mpya na kurithi mikoba ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa kazi Jumapili ya October 4 baada ya kutoka sare na wapinzani wao wa jadi Everton. Jurgen Klopp anajiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka mitatu, mkataba ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Jurgen Klopp baada ya kutua uwanja wa ndege jijini Liverpool akisindikizwa na John Lennon
Klabu ya Liverpool toka imeanzishwa imewahi kufundishwa na makocha 19 na sasa Jurgen Klopp ana ongezeka na kuwa wa 20. Kocha huyo wa kijerumani atatambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari Ijumaa ya October 9 katika mkutano na waandishi wa habari.
John Lennon akiwasli Hotelini

Note: Only a member of this blog may post a comment.