Issue za kuchafua mazingira kwa wenzetu
sio kitu cha mzaha kabisa, yani ukikamatwa kwa namna yoyote ile
unachafua mazingira basi watumishi wa serikali kwenye sekta husika
hawawezi kukuacha uende hivi hivi…
Weekend iliyopita rapper Wiz Khalifa alikuwa Pittsburgh kwa ajili ya kutoa show kwenye tamasha la Chuo cha Pittsburgh, ‘University of Pittsburgh Madness Basketball Event’… lakini alivyokuwa huko rapper huyo alinaswa akiwa anatoa haja ndogo nyuma ya bar moja iliyopo karibu na maeneo ya chuo hicho.
Kitendo hiko kikamfikia Msemaji wa Serikali za mtaa na Ulinzi wa Mazingira Sonya Toler na kupitia mtandao wa Associated Press, Sonya
alitoa onyo kwa rapper huyo huku akiuamuru kulipa fine kwani kitendo
alichokifanya kinachochea uchafuzi wa mazingira… isitoshe rapper huyo
alikutwa akifanya kitendo hicho akiwa na mwenzake ambaye alikuwa
ameshikia simu na kumpiga picha huku Wiz akiwa anacheka.
Wiz Khalifa
hakuishia hapo, baada ya kupewa onyo na kuamrishwa kulipa fine, rapper
huyo akaamua kupost picha hizi mbili kwenye page yake ya Instagram na caption iliyosema “I just love nature” na nyingine iliyosema “Have a great day” kama dharau dhidi ya onyo alilopewa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.