Brighton Masalu
SIKU Chache baada ya
muigizaji wa siku nyingi, Mahsein Awadhi Said ‘Dk. Cheni’ kutoa tamko
juu ya kumuoa ‘mtoto mkubwa’ katika tasnia hiyo, Elizaberth Michael
Kimemeta ‘Lulu’, binti huyo mwenye mvuto amesema hakuna mtu wa kumzuia
kuwa karibu na Dk. Cheni huku akishikilia alichokisema…. “mambo yetu
hayamhusu mtu”, Amani linaandika.
Muda mfupi baada ya Dk. Cheni kusema
haoni tatizo kwa kumuoa Lulu, gazeti hili lilimtafuta msanii huyo kwa
njia ya simu “Mtu anayesimama na wewe wakati wa shida ndiye rafiki kwa
kweli, Dk. Cheni amenisaidia pale ambapo kila mtu alijitenga nami, kama
kuna kinachoendelea kati yetu, ni cha kwetu na mambo yetu,” alisema.
Note: Only a member of this blog may post a comment.