Thursday, September 17, 2015

Anonymous

Watu Kelele Fisadi Fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza Kwani Kazi ya TAKUKURU au PCCB ni Nini? Mbona Hakamatwi


Fisadi
Watu kelele fisadi fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza kwani kazi ya TAKUKURU au PCCB ni nini? Nilidhani baada ya ripoti ya Mwakyembe hawa PCCB wangeifanyia kazi kuweza kufungua mashtaka. Kama chombo kama hiki akijaona umuhimu huo ufisadi ni upi? Serikali ni ile ile ya awamu ya nne na bado ina muda wa kuhakikisha wanatumia chombo chao PCCB kupata ukweli wa Richmond mbona nayo imekaa kimya? au inaamini hakukuwepo na wizi wa kodi za wananchi? Watanzania tusichanganywe na vitu visivyo na ushahidi wa kutosha au ushahidi butu. Nadhani neno ufisadi au Richmond ni lugha ya kampeni kama ilivyokuwa "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Achana nao wanaosema ni fisadi sikiliza Sera chagua kiongozi anayekufa. ##‪#‎Kiona‬ Mbali***

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.