Hamida Hassan
UBUNIFU! Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria
ameonesha kitu kipya baada ya kubuni namna ya kumsaidia mumewe, Henry
Kileo anayegombea ubunge Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro kupitia
Chadema, akisema anaomba michango kwa kutumia kadi maalum.
Akizungumza na gazeti hili, Joyce
alisema alilazimika kusambaza kadi hizo kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa
sababu hawana fedha za kampeni hivyo anaamini kwa njia hiyo anaweza
kumpiga tafu mumewe ili aweze kutimiza ndoto zake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.