MIONGONI mwa kazi ambazo tasnia ya filamu nchini inaweza kujivunia, ni hii ambayo imewajumuisha wasanii wenye majina waliotajwa hapo juu ambao kila mmoja kwa nafasi yake, amejitahidi kuitendea haki.
Ni wazo lililofanywa ili kuwaonesha watu madhara yanayoweza kuwatokea watu wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka ambao mara nyingi huupata kwa njia zisizofaa kama uhalifu au kushiriki matendo ya ushirikina.
Nimewahi kutabiri siku za nyuma kwamba Salim Ahmed ‘Gabo’ ana nafasi kubwa ya kuja kung’ara kama muigizaji nyota kutokana na uwezo wake katika kuigiza uhalisia wa mambo, kama alivyojitahidi kuonesha katika filamu hii, alipolazimika kumtongoza mama yake mzazi ili ashiriki naye mapenzi, kama sharti muhimu ili aweze kupata utajiri mkubwa.
Anajitahidi ‘kunata na beat’ katika vipengele vingi alivyoshiriki, sambamba na ‘mama yake mzazi’ Grace Mapunda ambaye naye amefanya vizuri sana katika nafasi aliyopangiwa, kwani alionesha jinsi gani alivyoweza kubadilika kutoka kuwa mama hadi mpenzi aliyekolea vibaya.
Lakini kama ambavyo inatokea katika filamu nyingi za Kibongo, zipo kasoro ndogondogo kadhaa ambazo zinapunguza uhondo. Mfano kuna siku Kajala alirudi nyumbani kwao kufuatia vitendo vya unyanyapaa alivyokuwa akifanyiwa na mama yake Gabo, ambapo alishtaki kwa mama yake mzazi.
Lakini baada ya mazungumzo na mama yake, akakubali kurejea nyumbani kwa mumewe. Lakini alipofika na kuingia chumbani kwake, akapigwa na mshangao kumkuta mumewe amelala na mama yake mzazi kitandani, kitu kilichomfanya aanguke na kupoteza fahamu.
Hapa kuna mambo mawili, kwanza ni vipi Gabo na mama yake waliamua kulala chumbani kwa mume wa mtu? Kwa kawaida, kitendo kama hiki kisingewezekana, kwani kwa tabia ambazo mama alikuwa akimuonyesha Kajala, tendo hilo lingeweza kufanyika chumbani kwa mama bila wasiwasi wowote.
Pia, ilikuwaje Kajala alipofika akakuta milango yote ipo wazi hadi chumbani? Maana kwa kuwa alikuwa ameondoka na tena imeshafika usiku, waliobaki nyumbani wangefunga milango ili kujihakikishia usalama, au zingeonekana juhudi za kumuona mtu akitafuta namna ya kuingia ndani na kuwafumania.
Lakini tatizo kubwa la filamu hii limeonekana mwishoni, kwani limekosa uhalali wa kuifanya kuwa laana. Gabo alikuwa anashiriki mapenzi na mama yake mzazi, sasa ili kuwaonesha watu madhara ya tendo hilo, ilikuwa vizuri kama tungeona mwisho usio mzuri wa utajiri uliopatikana kwa laana hiyo.
Kama siyo kupotea kwa utajiri huo, basi angalau tungeona mmoja wao au wote wawili wanatokewa na jambo lisilo la kawaida, ambalo lingeweza kuwa onyo kwa watazamaji na jamii kwa jumla kuhusu madhara ya kitendo hicho au hata utajiri wa kishirikina.
Lakini imeisha kwa watu hao kusameheana mbele ya mchungaji, kitu ambacho hakikai sawa. Halafu yule rafiki yake Gabo ameoneshwa kama mtu aliyefilisika, suala hapa nalo ni je, kafilisikaje? Na ikumbukwe yule hakuwa mhusika mkuu, watu walitaraji kumuona Gabo na mama yake wakiwa ndiyo waathirika wakuu wa filamu hiyo kutokana na wao kuwa ndiyo wahusika wakuu.
Vinginevyo kama nilivyosema mwanzo, ni moja ya kazi nzuri ambazo endapo watayarishaji wetu wataendelea kujifunza, uwezekano wa kuwa na ‘product’ nzuri sokoni ni mkubwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.