Imelda Mtema
Staa wa muvi Bongo, Ester Kiama
ameibuka na kusema kuwa wakati mastaa wenzake wakihangaika na kampeni za
siasa yeye anauza mkaa wake kwani amegundua kuwa wamemtenga kwa sababu
hawajawahi kumshirikisha kwenye lolote.
Akizungumza na Ijumaa,
Ester alisema kuwa awali alikuwa akiumia kuona ametengwa lakini
alipokaa na kufikiria kwa makini aliona ni bora alivyoachwa ili aifanye
kazi yake ya kuuza mkaa kwa ufasaha.
“Nilikuwa naumia na kusema nimetengwa
lakini wamenisaidia kwa upande mwingine, huu ndiyo wakati wa biashara
kwani mvua inakuja mpaka kampeni zinaisha nitakuwa nimeingiza fedha
nyingi kuliko waliojikita kwenye siasa,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.