Tuesday, September 8, 2015

Anonymous

VIDEO: VIONGOZI WA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM HUKO MOROGORO


Viongozi watatu wa Chadema wilaya ya Kilosa na mwanachama mmoja wametangaza kujiunga rasmi na CCM baada ya kuchoshwa na siasa za Chadema ambazo wameona hazina haki.
Viongozi hao waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa Ndugu Selemani Simba, Katibu wa Chadema wilaya hiyo Ndugu Ibrahim Abdallah Selemani, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Kilosa Kati Mussa Ngongo na aliyejitambulisha kama mwanachama kiherehere wa Chadema Bi.Oliver Mollel. 

Viongozi hao walitangaza kukihama chama cha Chadema kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Kilosa town.
Bonyeza play au download hapo chini kushuhudia video ya tukio hilo jinsi lilivyokua!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.