MALI za aliyekuwa
tajiri maarufu Dar, marehemu Charles John Mallya zimezua balaa baada ya
mke mkubwa, Philomena Masechu ambaye anadai kuchuma naye kiasi kikubwa
cha mali hizo kusema amedhulumiwa na mke mdogo, akimtaja Mariana kwa
kushirikiana na watoto wa wake wengine wa marehemu.
Akizungumza na gazeti hili kwa masikitiko, Philomena alisema
uchochezi mkubwa ulifanywa na watoto wa nyumba zingine ndogo (wake
wenzake).“Tangu ujana tulihangaika na marehemu na kufanikiwa kupata mali
nyingi, nikiwa kama mshauri wake lakini sasa watoto wa wake zake
wengine wawili waliyokuwa katika mikono yangu wamefikia hatua ya
kunidhulumu kila kitu. Hivi sasa naishi kwenye kijumba kidogo
nilichojengewa na ndugu zangu,” alisema mwanamke huyo huku akilia. Philomena aliendelea kusema kuwa, hitaji lake kubwa ni kupewa nyumba moja ya ghorofa iliyoko Sinza na nyumba ambayo haijaisha iliyoko Moshi, Kilimanjoro.Naye mmoja wa watoto wa mama huyo, Brighton Mallya akisimulia hali hiyo, alisema: “Baba aliacha mali nyingi na kutamka kuwa ni aseti ambayo kila mtu akipata shida ataweza kutatuliwa kupitia mali hizo kwa utaratibu na makubaliano, lakini sasa zimetekwa na baadhi ya ndugu.”
Baadhi ya mali alizoacha marehemu.
Aidha, kwa mujibu wa nyaraka hizo thamani ya mali hizo ni zaidi ya
shilingi bilioni moja na milioni mia tano (kwa mwaka 2010) ambapo
walalamikaji hao wanasema ilitakiwa kila mtu apate haki yake kama
inavyostahili na kusingekuwa na malalamiko. Akampa simu mwanaye wa kiume ambaye aliposomewa madai ya Philomena, alijibu: Iwe mwanzo na mwisho kupiga simu hii.”
Uwazi lilipohitaji ufafanunuzi zaidi alijibu yeye si mwalimu wa kufafanua.
Dawati letu lilifanikiwa kupata baadhi ya nyaraka zinazoonesha marehemu Mallya alizaliwa mwaka 1934, mwaka 1959 alioa mke mkubwa (Philomena) na walifanikiwa kupata watoto 6 na kuwa na biashara ya bar na hotel mjini Moshi.
Mwaka 1956 alimuoa Salome Gasper wakajaliwa kupata watoto wanne.
Note: Only a member of this blog may post a comment.