MLIPUKO wa ugonjwa wa kipindupindu
umeshika kasi sasa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Singida na
Mwanza baada ya kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi
kulazwa mahospitalini tangu ugonjwa huo uanze kusambaa kwa kasi nchini
mwanzoni mwa Agosti.
Hali inazidi kuwa mbaya katika maeneo
mbalimbali nchini kutokana na mlipuko wa kipindupindu, hali iliyopelekea
Shule nne za Msingi na moja ya Sekondari katika Kata ya Irugwa wilayani
Ukerewe mkoani Mwanza, kufungwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo
kisiwani humo.
Shule za msingi zilizofungwa ni za
Buruza, Nabweko, Sambi na Kulazu, wakati shule ya Sekondari ya Irugwa
zote zimefungwa leo baada ya wanafunzi 22 wa shule za Msingi Nabweko
kuambukizwa kipindupindu na watu wengine waliokuwa wanakusmbuliwa na
ugonjwa huo kufariki dunia.
Diwani wa kata hiyo ya Irugwa, Juma
Msongi ameithibitisha kuwa, tangu ugonjwa wa kipindupindu ulipoikumba
kata yake wiki iliyopita katika baadhi ya maeneo ya Kata hiyo, watu 8
wamefariki dunia na hali inazidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana kwa
huduma madhubuti za kuweza kukabiliana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa diwani huyo, kutokana na
hali ilivyo sasa wananchi wanatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira
ikiwemo matumizi sahihi ya vyoo na kujiepusha na ulaji ovyo wa vyakula,
kuhakikisha usafi wa mazingira, vyakula na kuchukua tahadhari juu ya
ugonjwa wa kipindupindu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.