Wanahabari wakichukua matukio.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) January Makamba, ambaye pia ni mjumbe wa
kamati ya kampeni CCM, ameshutumu kauli ya Katibu Mtendaji wa Baraza la
Habari MCT, Kajubi Mukajanga, kuwa Chama Cha Mapinduzi hakijathitisha
kushiriki mdahalo uliondaliwa kwa ajili ya wagombea nafasi ya urais.
Kiongozi huyo wa juu kisiasa ndani ya
CCM ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM yaliyoko jijini Dar es Salam,
kuwa chama chao kilipokea mwaliko wa MCT na kujibu kwa barua Septemba 13
mwaka huu.
Alifafanua kuwa barua hiyo kutoka CCM
ilijibiwa kwa kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 na kusainiwa na msaidizi wa
katibu mkuu , Stephen Msami, hivyo barua hiyo ikapelekwa kwa ‘dispatch’
ambayo nakala yake hadi sasa wanayo.
Makamba alisema kuwa baada ya hatua
hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana alifanya kikao cha pamoja
na wawakilishi wa MCT kwenye ofisi ndogo za Lumumba ili kutoa maoni ya
CCM kuhusu mdahalo huo.
Ameongeza kuwa CCM inasisitiza kwamba
John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea nafasi ya urais alikubali
kushiriki mdahalo wa wagombea wote hasa vyama vikuu katika nafasi ya
urais.
Tazama video ya taarifa hii hapa
Tazama video ya taarifa hii hapa
(Habari Picha: Haruni Sanchawa na Denis Mtima/ GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.