Wednesday, September 23, 2015

Anonymous

Mazoezi ya Kunyanyua Vyuma Yapelekea Kifo Cha Kijana Huyu Baada ya Moyo Wake Kupasuka…


Imekuwa kawaida kwa vijana wengi siku hizi kupenda kunyanyua vyuma ili kujenga mwili wenye misuli mikubwa na muonekano mzuri. Utamaduni wa kubeba vitu vizito ili kujenga mwili wenye muonekano flani wa kuvutia unazidi kushika kasi duniani kote licha ya vijana wengi Tanzania wameonekana kuanza kufanya mazoezi ya kubeba vyuma kwa miaka ya hivi karibuni.


Stori kutoka mtandao wa dailymail.co.uk umeripoti kifo cha Andrej Gajdos kijana mwenye umri wa miaka 19 na urefu wa futi 7 na inch 2, amefariki baada ya kubeba chuma na kupelekea misuli ya aorta katika moyo wake kupasuka. Andrej Gajdos alikuwa anaingia Gym mara mbili kwa siku na lengo lake lilikuwa kutengeneza mwili wake kuwa kama Dwayne Johnson.

Dr John Oxley ndio aliufanyia uchunguzi mwili wa Andrej Gajdos na kuthibitisha moyo wa Andrej Gajdos kuwa na uzito usio wa kawaida wa gram 680 wakati binadamu wa kawaida moyo wake unatakiwa kuwa na uzito wa gram 400 hadi gram 500, hata hivyo uchunguzi bado umeeleza Andrej Gajdos kuwa na matatizo ya mapafu kwani njia ya kupitisha hewa katika mapafu yake imetanuka. Andrej Gajdos ni raia wa Slovakia amekutwa na umauti akiwa Tesco Uingereza.


Dwayne Johnson.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.