KAMA kawaida yetu mpenzi msomaji wa kolamu hii tumekuwa tukikukutanisha na mastaa mbalimbali na kuweza kuwauliza maswali yanayohusu kazi zao na maisha yao ya kawaida nje ya sanaa.
Wiki hii tunaye staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka ambaye amefunguka mambo mbalimbali aliyoulizwa na wasomaji katika kolamu hii na kuyatolea ufafanuzi.
1.Msomaji: Nimekuwa nikisikia wasanii wengi wakilalamika kuwa, soko la filamu hapa Bongo bado halilipi wewe unalizungumziaje hilo na umenufaika vipi tangu ujikite kwenye sanaa? 0715413867.
Rose: Ukweli ni kwamba inategemea na juhudi za msanii mwenyewe jinsi unavyojituma basi utakula kwa urefu wa kamba yako kwani kwa upande wangu naona inalipa kiasi chake na binafsi nimenufaika kwani sanaa imebadilisha maisha yangu.
2.Msomaji: Dada Rose kwenye sanaa hapa nchini wasanii wa filamu mmekuwa mkisifika kwa tabia za umalaya kutotulia na bwana mmoja, unalizungumziaje hilo? 0765797352.
Rose: Kuna wachache wenye hiyo tabia ambao wanatuchafulia `cv,’ binafsi najiheshimu sana.
3.Msomaji: Niliwahi kusikia msanii hawezi kutoka mpaka atoe rushwa na ngono je, ulishawahi kuombwa rushwa ya ngono na changamoto hiyo ulikabiliana nayo vipi? 0717144016.
Rose: Hayo mambo yapo kwenye tasnia, lakini mtu anaponiomba rushwa ya ngono huwa naghairi kufanya naye kazi sababu kama ridhiki yangu ipo ipo tu siwezi kujidhalilisha.
4. Msomaji: Napenda sana kazi zako dada, ila nataka kujua wasanii wanapenda kuwa na mabwana ambao ni mapedeshee au kutoka kimapenzi na mastaa wenzao, wewe sifa za mwanaume unayaweza kuingia naye kwenye uhusiano ni zipi? 0716459807
Rose: Nashukuru kwa kunikubali, mimi napenda kuwa na mwanaume mwenye upendo wa kweli anayenithamini ambaye ni mchapakazi, pesa siyo kikwazo sababu hata mimi ni mtafutaji sijajibweteka kikubwa mtu athamini kazi yangu.
5. Msomaji: Ninavyofahamu umeachana na baba mtoto wako Malick Bandawe, changamoto gani unazokutana nazo kumlea mtoto mwenyewe wakati ulizoea malezi ya baba na mama? 0714474904.
Rose: Changamoto zipo, kuna wakati kuna mambo yanatokea labda mtoto kaumwa ilibidi kwa wakati huo nimsaidie nikiwa na baba yake lakini najikuta jukumu zima nikilibeba mwenyewe, ila nimeshazoea.
6. Msomaji: Hivi dada Rose ni kweli unatoka na Prodyuza Maneck kwani niliwahi kusikia ninyi ni wapenzi, au ukaribu wenu upoje? 0655 041689.
Rose: Hahaa Maneck ni mtu wangu wa karibu kwenye mambo ya kazi tu, isitoshe tunafahamiana kwa kipindi kirefu tangu mimi nikiwa nasoma Zanaki yeye Jitegemee.
7. Msomaji: Ni msanii gani unayemkubali kwenye ulimwengu wa filamu, ambaye pia ni mtu wako wa karibu hususan katika mambo ya kazi? 0712 561043.
Rose: Nitakuwa sijatenda haki nisipomtaja Ramy Garies (pacha wa Kanumba) ni kijana anayejituma sana, sababu hana kipindi kirefu kwenye tasnia lakini kazi zake kali sana naamini ataleta mabadiliko.
9.Msomaji: Tangu ujikite kwenye mapenzi ulishawahi kufumaniwa au kumfumania mpenzi wako, ulijisikiaje na ukachukua hatua gani? 0652 589202.
Rose: Sijawahi kufumaniwa, ila nilimfumania mpenzi wangu (hakutaja jina) nilipatwa na mshangao kisha nikachukulia kawaida tu kwa kuwa mapenzi ya Kibongo yamejawa na usaliti.
10.Msomaji: Nilikuwa napenda sana uhusiano wenu na Malick, ikiwa ni mwanaume mliyepanga kuingia kwenye ndoa mkabwagana je, una mpango wa kuingia kwenye ndoa kwa sasa? 0765652748.
Rose: Sifikirii swala la ndoa kwa kipindi hiki, sababu nilijisahau sana kwenye mapenzi kazi zikalala sitaki kurudia makosa sasa hivi nafanya kazi kwa bidii japo nina mpenzi na tuna malengo makubwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.