Nyota wa muziki wa Pop, Rihanna.
New York, Marekani
NYOTA wa muziki wa Pop, Rihanna hivi karibuni
alijikuta akiaibika mbele ya mashabiki wake baada ya kuvuja kwa kipande
cha video katika mitandao ya kijamii kikimuonyesha mpenzi wake mpya,
Travis Scott akitumia dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Katika kipande hicho cha video, Scott alionekana akiwa nyuma ya gari
akijidunga dawa hizo huku akiongea maneno akiuliza wako wapi marafiki
zake aliowataka kujitokeza waponde raha pamoja aliyokuwa anaipata wakati
huo.
“Scott siyo aina ya mtu wa kuwa na Rihanna, hakufanya chaguo sahihi,
ona anavyomuaibisha, bado ni mtoto kiakili,” aliandika shabiki mmoja
kwenye ukurasa wa Instagram wa Rihanna.

Note: Only a member of this blog may post a comment.