Msanii wa filamu za Bongo, Glasnost Kalinga akilia wakati marafiki zake wakitaharuki.
Mayasa Mariwata Na Shani Ramadhani
MSANII wa filamu aliyefahamika kwa jina la Glasnost Kalinga
hivi karibuni alipata aibu ya aina yake baada ya kulewa na kushindwa
kutembea.
Msanii huyo alinaswa na kamera yetu maeneo ya Afrikasana, Sinza saa 6
usiku ambapo alionekana akiwa amelala chini huku marafiki zake
wakijaribu kumkokota bila mafanikio.
Akizungumnza na Ijumaa katika eneo la
tukio, mmoja wa marafiki wa msanii huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe
gazetini alidai kuwa, hakuna chochote kibaya kilichompata ila alizidiwa
na pombe.
…Wote wakishangaana
“Hana tatizo, ni pombe tu ndiyo maana yuko katika hali hii. Tulitoka
vizuri viwanja tukiwa ndani ya Bajaj lakini tulipofika hapa na kushuka
tukashangaa mwenzetu kasinzia, tulipomuamsha akaonekana hajitambui,
aliposhuka ndiyo kashindwa kutembea,” alisema shosti huyo.
Baada ya paparazi wetu kunasa tukio hilo usiku, kesho yake asubuni
alimpigia simu Glasnost na kumuuliza ilikuwaje ambapo alisema kwa kifupi
kuwa hajui kilichotokea kwani ndiyo alitoka kuamka.
“Ndiyo nimeamka hapa, ila kwa kweli sijui hata kilichotokea jana ,”
alisema msanii huyo ambaye ameonekana kwenye filamu mbalimbali kama vile
Bikira, Mwadawa na nyinginezo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.