Wednesday, September 2, 2015

Anonymous

Pluijm Ataka Mabao 60 YANGA SC

pluijm2
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm
Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
KIPUTE cha michuano ya Ligi Kuu Bara, kinatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu, kwa timu 16 kuwania ubingwa wa ligi hiyo huku Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, akiweka bayana idadi ya mabao anayotaka.

Pluijm anataka kuiona timu yake ikitwaa tena ubingwa wa ligi hiyo msimu ujao na ili hilo litimie, amesema anataka kuwaona wachezaji wake wakifunga jumla ya mabao 60 au zaidi ya hapo ili kufanikisha lengo lao.

Hata hivyo, amesema pamoja na kutaka wote wafunge lakini jukumu zito anawapa washambuliaji wake wanne ambao ni Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Simon Msuva na Malimi Busungu.Wachezaji hao wamepewa majukumu hayo hivi karibuni baada ya kumueleza kocha huyo kuwa wapo tayari kubeba zigo hilo.

Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita kwa kufunga mabao 52 ikiwa ni idadi ya juu ukilinganisha na timu nyingine zilizokuwa zikishiriki ligi hiyo ambapo Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili, ilifunga mabao 36 na Simba ilishika nafasi ya tatu ikizifumania nyavu mara 38.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa kocha amewapa jukumu hilo na anaamini watalimudu.

“Ametutaka sisi kuwa viongozi wa kuhakikisha tunafunga mabao 60 au zaidi kwenye ligi kuu msimu ujao.
“Amesema kama tukifunga idadi hiyo, basi tutakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo mwishoni mwa msimu.
“Kutokana na hali hiyo kwa hesabu za harakaharaka, kila mmoja wetu anatakiwa afunge mabao 15, achana na yale yatakayofungwa na mabeki na viungo,” alisema Tambwe ambaye msimu uliopita alifunga mabao 14.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.