Rapa Lil Wayne akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Christina Milian.
New York, Marekani
SIKU chache baada ya kutangaza kuvunja uhusiano wa
kimapenzi uliodumu kwa mwaka mmoja, imebainika kuwa rapa Lil Wayne na
Christina Milian hawajatengana katika masuala ya kikazi.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa wasanii hao, zimeeleza kuwa
uhusiano huo ulivunjika wiki iliyopita lakini bado Christina ataendelea
kuwa memba wa lebo ya Young Money ambayo ipo chini ya Lil Wayne.
Hata hivyo hiyo siyo mara ya kwanza kwa mwanamama huyo kutengana na
wapenzi wake wa kiume tangu alipotalikiana na aliyekuwa mumewe The
Dream.

Note: Only a member of this blog may post a comment.