Pirika za asubuhi ni nyingi na pengine muda wa kusikiliza uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, kazi yangu ni kuhakikisha zile kubwa kubwa za leo zinakufikia…
NEC imesema hakuna kura zitakazoibiwa hivyo wagombea waache kuwatisha wananchi, Magufuli ameahidi
kuondoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji wa kubwa, ahaidi pia wanafunzi
wa darasa la kwanza hadi kidato cha 4 kusoma bure.
Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa ahaidi elimu bure mpaka chuo kikuu, kutafuta suluhisho la foleni Dar es salaam na kuondoa ushuru wa mazao… Mgombea Urais kupitia Chama cha CUF Maalim Seif asema ataifanya Zanzibar kuwa Singapore ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar.
Wasomi na waharakati wamshukia Askofu Gwajima waiomba Serikali kuwapiga marufuku viongozi wa dini kujihusisha na siasa, Gwajima kupandishwa kizimbani leo Mahakama ya Kisutu, na mambo saba yammaliza Dk. Wilbroad Slaa kisiasa.
Mufti wa Tanzania kupatikana leo jijini Dodoma, Maaskofu waipongeza NEC na walemavu wataka wakalimani wa lugha za alama kwenye kampeni za wagombea.
Kama uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ulikupita asubuhi hii, hapa chini nimeiweka sauti yake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.