Sunday, September 6, 2015

Anonymous

MSIBA: Mwanadamu Mfupi Zaidi Duniani Afariki -PICHAZ


Ilipofika mwaka 2012,Chandra Dangi aliwekwa katika rekodi za kitabu cha Guinness kama mtu mfupi zaidi duniani akiwa na kimo cha nchi 21.5 sawa na futi 1.41
Mwanadamu anayeshikilia rekodi ya kuwa mtu mwenye kimo kifupi zaidi duniani, Chandra Dangi, wa nchini Nepal ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 75 kwa Ugonjwa wa Pneumonia.

Chandra Dangi akiwa ananyoa ndevu zake
Kifo hicho kilitokea Ijumaa asubuhi, katika hospitali ya Lyndon B. Johnson Tropical Medical Center iliyoko katika visiwa vya American Samoa.

Mr Chandra akipanda ngazi
Ilipofika mwaka 2012,Chandra Dangi maarufu kama Price Chandra, mwenye kimo cha nchi 21.5 sawa na futi 1.41 alivunja rekodi ya kitabu cha Guinness

Chandra akiwa amesimama na Sultan Kosenambaye anashikilia rekodi ya mtu mrefu zaidi duniani katika kimo cha futi 8.1
iliyokuwa ikishikiliwa na marehemu Gul Mohammed wa New Delhi, India, aliyekuwa na kimo cha nchi 22.5 sawa na futi 1.47.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.