Aeleza alivyoanza kuugua hadi alipo sasa
Na Haruni Sanchawa
MWANAMKE mmoja, Emakulata John, 28, amekuwa
akiugua kwa miaka zaidi ya kumi bila msaada wowote wa uhakika wa
kitabibu na hali yake kwa sasa ni mbaya, hivyo kuwalilia Watanzania ili
waweze kuokoa maisha yake.
Hivi
sasa Emakulata hasikii, haoni vizuri wala hawezi kutembea kutokana na
maradhi yaliyomuandama kwa kipindi kirefu sasa na kusababishia kuwa ni
mtu anayeshinda kitandani kutokana na kile alichodai kuwa mwanzo
alitakiwa alipie gharama za tiba zilizogharimu Sh. 60,000 lakini akawa
hana.
Mgonjwa huyo hasikii na ili uweze kufanya naye mawasilinao ni lazima
umwandikie kwenye karatasi aisome kisha aanze kukuelezea hali ambayo ni
ngumu sana katika maisha ya mwanadamu kama msichana huyo anavyoishi.
“Kwa sasa naishi na mtoto wa dada yangu karibu na Chuo Kikuu cha
Kampala kilichopo Gongo la Mboto. Nimezaliwa miaka 28 iliyopita na
kuanza shule hadi kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kigoma
iliyopo mkoani Kigoma mwaka 2004, nilikuja Dar es Salaam na kufikia
Ubungo na kuanza kozi ya kompyuta.”
CHANZO CHA UGONJWA
“Wakati nikiwa nasoma kompyuta ghafla nikaanza kuumwa, nilipokwenda hospitali kupimwa vipimo vikawa havioneshi nina tatizo gani.
“Nikiwa naendelea na harakati za kujitibu hali ilizidi kuwa mbaya
miguu ikawa mizito na kufa ganzi, mgongo ukawa unauma bila kujua tatizo,
hiyo ilikuwa kabla ya mwaka 2004.
“Mwaka 2005 ndipo tatizo lilipojulikana baada ya kuomba msaada kwa
watu nikafanyiwa vipimo tena na kuambiwa kuwa nina tatizo kwenye ubongo
wa nyuma.
SH.60,000 HAKUWA NAZO
“Baada ya hali hiyo kubainika niliambiwa gharama ya matibabu na
vipimo mwaka huo kwa ujumla ilikuwa Sh. 60,000 lakini nikawa sina na
nilikosa msaada kutoka kwa watu ambao nilikuwa nikiwategemea.
“Kutokana na hali hiyo kuumwa nilisitisha masomo ya kompyuta ambayo
nilikuwa nikisoma Ubungo jijini Dar es Salaam na kuhamia Kigamboni kwa
dada yangu (jina tunahifadhi) ili niweze kupata msaada wa karibu lakini
ilikuwa ni kinyume na nilivyokuwa ninategemea kwa sababu dada
hakunihudumia ipasavyo.
“Ubinadamu ni kazi sana (analia kisha akasitisha kuongea kwa muda wa
dakika tano) nalia kwa sababu dada yangu alinifanyia ukatili, aliniacha
naumwa na nakosa usingizi kutokana na maradhi haya.
GHARAMA ZA TIBA ZAPANDA
“Baada ya kuhangaika sana mwaka jana nilipima tena kwa msaada wa watu
ikabainika kuwa nina uvumbe mkubwa sana kwenye makalio kupitia uti wa
mgongo na madaktari waliniambia kuwa gharama ya matibu ni Sh. 800,000
kwa kuanzia.
“Sasa kama nilishindwa kulipa shilingi 60,000 hizo laki 800,000
nitazipata wapi (analia), elfu sitini tu zinanipeleka kaburini,
ningekuwanazo mwanzo isingefikia gharama hii.
“Nimehangaika sana, nimetibiwa hospitali kwa misaada ya watu,
nimetibiwa Bochi Medical Center iliyopo Mbezi Kwa Msuguli na kubainika
kuwa nina moyo mkubwa, vifundo vimepishana na ndiyo chanzo cha kupooza.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane na mgonjwa
huyu kwa namba ya simu 0719 464341 na mawasiliano hayo yafanywe kwa njia
ya ujumbe yaani (SMS) kwani hasikii. Msichana huyo ni yatima.
Note: Only a member of this blog may post a comment.