Wasichana warembo wanaomchukulia Rihanna kama mfano wa kuigwa na
kujaribu kufanya kile anachofanya kuanzia mavazi, muonekano na mengine
wanaweza kuwa wanapotea kwa kuwa yeye anajielewa sio mtu sahihi kwenu.
Mwimbaji huyo ameeleza wazi kuwa yeye sio mfano wa kuigwa katika
jamii (role model), katika mahojiano maalum aliyofanya na jarida la NME.
Kauli hiyo ya Rihanna ilifuatia maswali yaliyolenga kufahamu msimamo
wake kama angefanya ziara ya muziki na mwimbaji mwenzake Taylor Swift
ambapo akataa na kudai kuwa hawaendani hata kidogo. Alisema yeye na
mwimbaji huyo wanatofautiana sana kwa kuwa Tailor ni mfano wa kuigwa na
yeye sio.
Ni kama Rihanna amewaelekeza wanaotafuta mfano wa kuigwa katika jamii kumfuata Taylor Swift badala ya kumfuata yeye.
“’I don’t think our brands are the same: I don’t think they match, I
don’t think our audiences are the same. In my mind she’s (Taylor) a role
model, I’m not,” alisema Rihanna.

Note: Only a member of this blog may post a comment.