Thursday, September 17, 2015

Anonymous

MAINDA Akataa Mamilioni ya UKAWA, CCM

maindasuka.jpg
Brighton Masalu
SITAKI! Staa wa muda mrefu katika tasnia ya uigizaji Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amekataa vishawishi vya kujiunga na vyama vya siasa, ikiwa ni pamoja na fedha zinazofikia mamilioni alizoahidiwa na wapambe wa vyama hasimu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chadema kinachowakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Risasi Mchanganyiko lina mkanda mzima. 

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu, Mainda aliyejipambanua kuwa hana chama, alisema baadhi ya wasanii wenzake ambao wako ndani ya vyama hivyo, walijaribu kutumia mbinu nyingi kuhakikisha anakuwa mwenzao.
Msanii huyo ambaye kwa sasa ameokoka, alisema kilichomfanya kukataa kujiunga ni kwa vile hana uelewa wa kutosha juu ya siasa hivyo hawezi kufuata mkumbo kama wanavyofanya baadhi ya mastaa wenzake. 

“Mimi sina chama kabisa, ni raia wa kawaida, siku ya uchaguzi nitajitokeza kupiga kura, na suala la nani nitamchagua inabaki kuwa siri yangu kama jinsi katiba inavyoelekeza kuwa kura ni siri ya mpiga kura mwenyewe.
“Japo nimepitia vishawishi nimekataa kabisa, pamoja na kutojua siasa lakini pia nina kazi nyingi, ninachoweza kusema ni kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na amani ya nchi itakuwa palepale, mtu asikubali kupiga kura kwa kushawishiwa kwa pesa, aamue mwenyewe,” alisema Mainda.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.