Jana, Septemba 20 ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya Diamond
Platinumz na mashabiki wake waliposherehekea siku ya 40 ya mtoto wake
‘Tiffah’ tangu alipozaliwa.
Sherehe hiyo pia iliambatana na kuoneshwa hadharani kwa mara ya
kwanza kwa mtoto huyo ambaye amekuwa maarufu na milionea akiwa bado
mchanga.
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali kuwa kuna kiasi cha fedha ambacho
kimewekwa na Diamond Platinumz kwa ajili ya watu ambao wangependa
kumuona Tiffah uso kwa uso.
Hata hivyo, Diamond Platinumz ameiambia BBC kuwa taarifa hizo ni za
uongo na kwamba hakuna gharama yoyote ambayo mtu anapaswa kulipia kwa
kumuona mtoto huyo ambaye picha yake ya kwanza inayoonesha sura yake
hadharani ilidhaminiwa na benki kubwa nchini.
Katika hatua nyingine, Diamond alieleza sababu zilizopelekea
kumfungulia binti yake huyo akaunti ya Instagram tangu akiwa tumboni.
“Ulimwengu wa mitandao sasa hivi, ulimwengu unakua na unavyomkuza
mwanao lazima umtengeneze mapema, umtengenezee mazingira ya kuwa brand
mapema hususan sisi watu maarufu. Na namshukuru Mwenyezi Mungu tangu
siku aliyozaliwa hadi sasa hivi siku zinavyozidi kwenda anazidi kuingiza
[pesa]. Ni mtu anayeingiza hela japokuwa hajaanza kuwa na ufahamu
wake,” Diamond aliiambia BBC.

Note: Only a member of this blog may post a comment.