KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Iringa,
Ramadhani Mungi, amesema Jeshi hilo linamshikila aliyekuwa Mbunge wa
Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na wenzake 61
kwa tuhuma za kufunga barabara ya Kihesa mjini Iringa.
Akizungumza kwenye kikao cha dharura na
waandishi wa habari kwenye kijiji cha Migori kilichopo Jimbo la Isimani
mkoani Iringa, RPC Mungi alisema Jeshi hilo lilimtia nguvuni Msigwa na
wenzake hao jana Jumatatu majira ya jioni.
Ilikuwa ni baada ya kupata taarifa kuwa
watu hao walifunga barabara ya Kihesa wakiwazuia watu waliokuwa wakienda
kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli uliokuwa ukifanyika katika
viwanja vya Samora mkoani Iringa.
HABARI NA RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO IRINGA

Note: Only a member of this blog may post a comment.