Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo imefutilia mbali mashtaka mawili ya
ubakaji yaliyokuwa yanamkabili muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel
Mbasha.
Mbasha alikuwa akikabiliwa na mashataka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Katika shitaka ya kwanza, mbasha alidaiwa kumbaka shemeji yake huyo Mei 23, 2014 katika eneo la Tabata, Kimanga. Na katika shitaka la pili, Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo ndani ya gari aina ya Toyota Ipsum.
Ilidaiwa kuwa Mbasha alifanya vitendo hivyo wakati ambapo alikuwa na matatizo na mkewe Flora, akimtuhumu kuisaliti ndoa yao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.