Ni kawaida kwa msanii kujikuta anatokwa machozi awapo jukwaani hasa
anapoimba wimbo wa hisia ambao kwa namna moja ama nyingine unamletea
kumbukumbu ya tukio fulani.
Paul Okoye wa P-Square pia hutokwa machozi jukwaani mara nyingi wanapoimba hit song yao ‘Beautiful Onyinye’.
Weekend iliyopita, Septemba 5 mapacha hao wa Nigeria walianza ziara
yao ya Marekani na Canada kwa kutumbuiza Washington Dc, na wimbo huo
ulimtoa machozi tena na kuamua kuandika kitu kwenye Instagram yake
kuelezea kwanini huwa analia mara kwa mara anapouimba.
Paul amepost picha yake akiwa anatokwa machozi na kuandika kuwa
‘Beautiful Onyinye’ ndio wimbo uliokuwa ukipendwa zaidi na marehemu mama
yao, ndio maana mara nyingi huwa anajikuta analia jukwaani kila
wanapouimba.
“Sometimes I cry on stage, especially when singing beautiful
onyinye, our late mum’s favorite song ….. I know she’s watching with
our dad. Miss u guys….. DC 1 luv”
Mama yao Mrs Josephine Okoye alifariki dunia Jumatano ya July 11, 2012.
‘Beautiful Onyinye’ inapatikana kwenye album yao ya mwaka 2011 The Invasion.

Note: Only a member of this blog may post a comment.