Wakati kikosi cha Simba SC kinaondoka leo kwenda Zanzibar kuweka kambi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amewaambia mahasimu, Yanga SC wasubiri supu ya mawe kwa kachumbari ya pilipili manga na tomato Jumamosi wiki hii.
Yanga imezifunga Coastal Union 2-0, Prisons 3-0 na JKT Ruvu 4-1 juzi, wakati Simba SC imezifunga 1-0 African Sports, 2-0 Mgambo na jana 3-1 Kagera Sugar.
Na Hans Poppe amesema baada ya ushindi wa 3-1 jana sasa wanakwenda kambini Zanzibar kuiandalia Yanga SC ‘dozi nene’ na amewataka wapinzani wao hao wa jadi wakae tayari.
“Yanga SC wanapiga sana kelele, imekuwa timu ya magazetini, inasifiwa sana wakati uwanjani haina lolote. Sasa wasubiri supu ya mawe iliyochanganywa na kachumbari, pilipili manga na tomato Jumamosi,”amesema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.