Ikiwa ni katika muendelezo na harakati za kuipeleka klabu ya soka ya Simba katika mfumo wa kisasa na kujenga kikosi chenye wachezaji wenye morali uwanjani, mwezi September klabu ya Simba imetangaza kuanzisha mfumo wa kumtafuta mchezaji bora wa mwezi.
Kupitia kwa Rais wa klabu hiyo Evans Aveva
ametangaza kuanzisha mpango huo mwezi September, ambapo mfumo
utakaotumika kumpata mchezaji bora wa mwezi ni mashabiki ndio watakuwa
na nafasi ya kumchagua kwa kumpigia kura kwa njia ya sms.
“Wanachama
na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika
kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa
klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
Tunaamini kuwa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza
morali na kujituma kwa wachezaji wetu” >>> Evans Aveva
Note: Only a member of this blog may post a comment.