TADIP ni taasisi isiyokuwa ya 
kiserikali iliyosajiliwa mwaka 2006, miongoni mwa shughuli kuu za 
taasisi hiyo ni utafiiti na ushawishi wa sera na sheria nchini 
Tanzania.Tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ikileta chachu katika maendeleo
 ya Tanzania.
Kupitia taasisi hiyo leo Sept 25 ilikutana na waandishi wa habari 
kuelezea tafiti zilizofanyika katika chaguzi hizi zinazoendelea 2015, 
kwa mujibu wa mkurugenzi wa bodi ya TADIP George Shembusho..’Wananchi
 waliulizwa ni mgombea yupi wangemchagua kuwa rais ikiwa uchaguzi 
ungefanyika siku ambayo taarifa za utafiti huu zilizopokuwa zinakusanywa
 (wiki tatu za mwanzo, Septemba).Asilimia 54.5% ya washiriki walijibu 
kwamba wangemchagua Edward Lowassa, asilimia 40% wangemchagua Dkt. John 
Pombe Magufuli huku asilimia 2% walisema wangemchagua Anna Mghwira’ -George Shembusho
‘Wengine ni Hashimu Rungwe (0.4%) na 
Chief Yemba (0.1%) huku 3% wakiwa wamesema hawajui wangemchagua 
nani.Edward Lowassa anaungwa mkono zaidi mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, 
Arusha na Dar huku Dkt. John Magufuli akikubalika zaidi katika mikoa ya 
Dodoma na Morogoro kama inavyoonekana kwenye graph nambari 6′ –George Shembusho
‘Kwa upande wa makundi ya umri, Edward Lowassa anaonekana kuungwa 
mkono zaidi na vijana pamoja na watu wenye umri wa kati (Miaka 18- 47), 
watu wazma wenye umri juu ya miaka 47 wanamuunga mkono zaidi Dr. John 
Magufuli’ – -George Shembusho
-via millardayo 
 

 
 
 
 
Note: Only a member of this blog may post a comment.