Saturday, September 26, 2015

Anonymous

Maneno ya BEN POL Kutokuwepo Kwenye Jukwaa Lolote la KISIASA Yako Hapa…

Katika  baadhi ya wasanii ambao hawajaona wakiwa kwenye jukwaa lolote la kisiasa kuwasaidia wagombea kunadi sera zao ni star wa RNB Ben Pol. 
 
Mkali huyo alipofika leo Sept 25, 2015 katika studio za Ayo TV pamoja na millardayo.com alisema…’Kusema kweli nimekuwa mzito sana kuona kama ni sawa au sio sawa yaani nimekuwa mtu ambaye niko slow sana unakutana kuna wakati hata mtu akiniuliza Ben unafanya kampeni moyoni mwangu unakutana inanichukua muda mrefu kumjibu lakini sijapata majibu mpaka sasa mimi naangalia tu kama shabiki naona tu watu wana post huyo mara huyo- Ben Pol 

‘Kwa mwaka huu hivi vitu vinachanganya sana na sijui labda mpaka tusubiri tarehe 25 October nitapata ufumbuzi kamili kwenye kile chumba cha kupigia Kura, lakini kuna wakati baadhi ya wabunge wanaogopa unakuta mbunge akinitumia SMS kuhusu kum support kwenye kampeni yake anasita kutoka na msimamo wangu niliojiwekea yaani uchaguzi wa mwaka huu una changamoto nyingi sana’ – Ben Pol
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Ben Pol

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.