Ni kawaida kwa mtu kuwa rafiki wa mpenzi wake kwenye Facebook au
kumfollow kwenye Instagram lakini mtaalam wa masuala ya mahusiano
ameonya kuwa hiyo inaweza kuwa na athari kubwa.
Kwa mujibu wa Ian Kerner wapenzi ambao hawafuatani kwenye mitandao ya kijamii wana asilimia kubwa zaidi ya kuwa pamoja.
Mtaalam huyo mwenye makazi yake jijini New York amedai kuwa kuacha
kumfuata mpenzi wako kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kuimarisha
zaidi uhusiano wako.
Amesema matumizi ya simu yanamaanisha kuwa wapenzi hutumia muda
mchache kuzungumza ana kwa ana na hivyo kusababisha kutokuelewana na
majibizano.
Kwa mujibu wa utafiti wa Pew Research Center, asilimia 25 ya watu
walioana au kuishi pamoja wamewahi kuwatumia ujumbe wa simu wapenzi wao
ilhali wakiwa pamoja ndani.
Idadi hiyo pia ilihisi kuwa wenza wao waliwahi kukerwa na simu zao na
asilimia 8 wamewahi kubishana kuhusiana na muda wa wenzi wao wanaotumia
mtandaoni.
Kerner, ambaye kwa sasa ameifuta akaunti yake ya Facebook amedai kuwa
wakati alikuwa nayo naye pia alikutana na changamoto kadhaa kwenye ndoa
yake.
Chanzo: Mail Online
Chanzo: Mail Online

Note: Only a member of this blog may post a comment.