Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ametoa taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Arsenal Danny Welbeck… Wenger alikuwa na matumaini ya kuwa Welbeck atarejea Uwanjani baada ya mapumziko mafupi ya Ligi yaliyofanyika ili kupisha mechi za Kalenda ya FIFA weekend hii.
Lakini taarifa mpya zinaeleza ili Welbeck
awe sawa baada ya kupata majeruhi ni lazima afanyiwe upasuaji katika
goti lake la kushoto ambapo upasuaji huo utamuweka nje ya uwanja kwa
muda kiasi. Licha ya Wenger kuthibitisha, taarifa hizo ni pigo kwani Arsenal haijafanya usajili wa mshambuliaji yoyote.
Licha ya taarifa hizo pigo kwa Wenger bado mashabiki wa Arsenal na katika mitandao ya kijamii wanaelekeza malalamiko yao kwa Wenger, kwani kama angefanya usajili wa mshambuliaji mwingine isingekuwa kuna pengo kubwa la kumkosa Welbeck.

Note: Only a member of this blog may post a comment.