Msanii wa filamu za Bongo, Kajala Msanja na mwanaye Paula.
Imelda Mtema
Chumba cha mtoto wa prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse
‘P- Funk’ na Kajala Msanja, Paula kimeibua mshituko kufuatia namna
kilivyosheheni vitu vya thamani.
Juzikati
mwandishi wetu alitinga ndani ya mjengo anaoishi Kajala maeneo ya
Mwenge jijini Dar na kustaajabu mengi lakini miongoni mwayo ni chumba
ambacho ametengewa Paula.
Chumba
hicho kina kitanda cha gharama, kimerembwa kwa kuandikwa jina la Paula
ukutani, kuna kabati kubwa la nguo na shelfu iliyosheheni viatu kibao
vya kila aina.
Hata hivyo, ikabainika kuwa, kufuru zilizomo chumbani kwa binti huyo
anayesoma zinatokana na mama yake ambaye pesa inaonekana kuwa siyo shida
kwa muda huu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.