Imelda Mtema
Mambo ya ndoa! Mwigizaji wa kitambo ambaye ni zao la kundi la zamani
la Nyota Ensembels lililokuwa likirusha michezo yake kupitia Runinga ya
ITV, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa yeye ni msanii lakini maisha
ya kisanii hayapeleki kwenye ndoa yake kwani ndoa siyo mambo ya ‘action
and cut’ kama wanavyofanya lokesheni.
Mwigizaji wa kitambo, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Cathy ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, ndoa nyingi za mastaa huwa
hazidumu kwa sababu huchukua maisha ya nje ya ndoa na kuyapeleka kwenye
ndoa ndipo wanapojikuta wakishindwa kudumu ndani ya ndoa kwa muda mrefu.“Maisha ya ndoa hayahitaji mambo ya kisanii kabisa kwa kuwa wanaume wengi hawapendi mambo hayo,” alisema Cathy.

Note: Only a member of this blog may post a comment.