Kampuni ya Apple imeonesha simu zake mpya, iPhone 6s na 6s Plus kwenye tukio lililofanyika jijini San Francisco Jumatano hii.
Simu hizi pamoja na mambo mengine zina teknolojia iitwayo 3D Touch.
3D touch screen zinamsaidia mtumiaji wa simu kubonyeza screen kwa
nguvu kupata menu zaidi ama vitu vya ziada vya picha za selfie.
Simu hiyo pia ina chip inayodaiwa kuwa ya haraka zaidi katika
teknolojia ya simu za mkononi. Camera za simu hizo zimeongezewa uwezo
zaidi wa megapixel 12 inayotoa picha zenye ubora zaidi na ambayo inaweza
kurekodi video zenye ubora wa 4K.
Camera ya mbele ya simu hiyo ina 5mp ili kuboresha ubora wa picha za
selfie na ambayo ina flash. Kuna teknolojia mpya ya ‘live photo’ ambayo
huchanganya picha na video.
Kwenye tukio hilo pia kampuni hiyo imezindua iPad mpya na kubwa iitwayo iPad Plus.
CEO wa Apple, Tim Hook akionesha iPad mpya
CEO wa Apple, Tim Cook alionesha pia tablet mpya na Apple TV mpya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.