Monday, September 21, 2015

Anonymous

AJALI: Wanafunzi Wagongwa na Gari Wakiwa Katika Bajaji Jijini Dar [PICHAZ]


Mwanafunzi wa Sekondary ya Loyola akipelekwa kwenye gari kuelekea Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana mchana, baada ya bajaj yenye namba za usajili MC 402 AWD waliokuwa wameikodi na wenzake Bandarini wakitokea Zanzibar kugongwa na Pickup Double Cabin yenye namba DFPA 826 katika makutano ya barabara ya Sokoine na Azikiwe jirani na Benki ya NBC. Katika ajali hiyo wanafuzi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo.

Wanafunzi wa shule hiyo wakimfariji mwenzao Martha Silayo (katikati), aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Wananchi wakiangalia bajaj iliyogongwa. Imeelezwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa bajaj hiyo ambapo pia dereva wake alijeruhiwa.

Askari wa usalama barabarani na wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali hiyo.

Bajaj iliyogongwa ikiwa eneo ilipopatia ajali 'Kweli BOGOTI imegongwa'
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.