Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana alikuwa mstari wa mbele kunogesha kampeni za mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli,
akisisitiza ni chaguo sahihi kwa Watanzania na kwamba hata upatikanaji
wake ulikuwa sahihi kwa asilimia 100 na kwamba, yeye aliyekuwa mjumbe wa
vikao hivyo ni shuhuda wa hilo.
Katika Uwanja wa Nelson Mandela, Pinda alisema kuna baadhi wamesusa na hivyo haya yeye alipokosekana katika uzinduzi wa kampeni za Urais za CCM jijini Dar es Salaam, kuna waliompigia simu na kuhoji kwa nini hakuwepo.
“Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Kamati ya Maadili, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Nimeona nisiache kuja huku, maana Waswahili hawaachi kusema, unaona hata Waziri Mku kamsusia mwenzake, maana alikuwa naye katika kinyang’anyiro…Mimi ni muumini wa chama changu, kilichofanyika mpaka tukampata Magufuli nataka niwaambie ni halali asilimia 100,” alisema.
Alifafanua kuwa walichokuwa wakitafuta CCM ni kumpata mtu ambaye kwa wale waliokuwa katika kamati na vikao hivyo, wamekubaliana kuwa anaweza kuwavusha bila matatizo.
“Mimi nilikuwepo na nilikuja mkanidhamini na niliwaambia tulikuwa 42, ikaja 38 nikasema atabaki mmoja. Tumeletewa Magufuli, si mwingine si Pinda. Chama hapo kama ni kupiga, basi kimelenga shabaha. “Huyu baba ni mwadilifu na mchapakazi sana, ana huruma sana lakini kwa mambo yenye uongo, wakwepa kodi, wezi ni mkali sana…
Nilitaka kuja kuwathibitishia kuwa mimi nimeungana naye kwa asilimia mia,” alisema. “Juzi mtu mmoja alinipigia akasema mbona katika uzinduzi hukuwepo, nikamjibu kwa hiyo?” nikahoji. Akaongeza: “Tumepewa heshima ameanzia huku Katavi na Rukwa, namngoja huku.
Sisi barabara tumepata, mkoa wa Katavi tumepata wilaya na kata za kutosha, sasa zawadi ni kumpa kura”. Wapanda daladala Alisema anashangaa imekuwaje watu waanze kupanda daladala sasa kwenda Chanika na kwingineko Dar es Salaam na kuhoji; “Siku zote alikuwa wapi.
Anangoja moto umewaka ndio anapanda?” Magufuli Akizungumza katika mkutano huo, Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli alianza kwa kusalimia kwa karibu lugha kumi na kusema ataunda serikali ya mawaziri wachache, lakini kazi atakazowapa anahisi baadhi watakimbia. Aliahidi kuhakikisha wafanyabiashara wadogo hawabugudhiwi, wakiwemo bodaboda na mamalishe na kuhakikisha wafanyabiashara wakubwa wanalipa kodi ili ihudumie wananchi.


Note: Only a member of this blog may post a comment.