Friday, August 7, 2015

Anonymous

Wafahamu Wasanii wenye misamiati mingi zaidi kwenye Hip Hop Marekani ni…? Wajue hapa.


Nimekutana na stori kwenye moja ya mitandao inayoonyesha wanamuziki wa hip hop Marekani Eminem, Kanye West na Jay Z wanafanana kitu kimoja…utumiaji mwingi wa misamiati mikubwa kwenye nyimbo zao.

Eminem
Kutokana na utafiti mpya uliofanyika, wasanii hawa wa tatu ni miongoni mwa wasanii 5 bora wenye misamiati mingi zaidi kwenye industry ya muziki Marekani. “Nia ni kulinganisha ukubwa wa utumiaji wa misamiati wa hawa wananuziki” utafiti huo unasema.

Jay Z

Kuna baadhi yao wamefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki mpaka leo kwasababu ya sanaa yao na jinsi ambavyo wameweza kutumia misamiati kuwagusa mashabiki…Utafiti huo umetumia orodha ya wasanii 99 bora duniani, wamelinganishwa na kuchujwa kwa kuhesabu idadi ya misamiati ya kipekee waliotumia kwenye nyimbo zao zote.

Kanye West
Eminem aliibuka kidedea akiwa na idadi ya misamiati 8,818 ya kipekee kwenye nyimbo zake akifuatiwa na rappa Jay Z akiwa na idadi ya misamiati 6, 899 , Marehemu Tupac Shakur akiwa na idadi ya misamiati 6,569 na Kanye West akiwa na idadi ya misamiati 5,069.

2 Pac
Mtunzi wa nyimbo Bob Dylan ameshika nafasi ya 5 akiwa na idadi ya misamiati 4,883 na ni msanii pekee asiyefanya muziki wa hip hop kushika nafasi hiyo. Kitendo cha wasanii wa Hip Hop kushika nafasi zote 4 za juu pengine sio kitu cha kushangaza sana kwani wengi tunafahamu kuwa asili ya muziki wa Hip Hop umejengwa kwenye misingi ya kutumia mistari yenye misamiati migumu.

Bob Dylan
Wewe unauonaje uchambuzi huu mtu wangu? unakubaliana na hii orodha ama unahisi ni msanii gani wa Hip Hop Marekani anatakiwa pia kuwepo kwenye hii 5 bora?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.