Friday, August 7, 2015

Anonymous

LIPUMBA na CUF ndio basi, UKAWA je? Wasanii na kikao cha TCRA? Wabunge Walioanguka? (Audio)

Magazeti ya Ijumaa 7 August 2015 yako mtaani tayari na vichwa vyake vikubwa vya habari, kazi yangu ni kukusogezea zile zote zinazoweka headlines magazetini… ziko na hizi zilichochambuliwa Redioni. 

Prof. Ibrahim Lipumba ang’oka hali tete UKAWA, ajiuluzu Uenyekiti wa CUF akimpinga Edward Lowassa adai UKAWA washindwa kuenzi uadilifu na uzalendo… CCM kuwapitisha Wagombea Ubunge Z’bar leo… Edward Lowassa aipasua vipande UKAWA… NEC yaonya kampeni nyumba za ibada…Siri yafichuka CUF watoa tamko na kuna stori pia ya mke wa Dk. Wilbroad Slaa kufunguka. 

Idadi ya Wabunge 51 waanguka Kura za Maoni ndani ya Vyama vyao… Zaidi ya majambazi 10 waliohusika na tukio la Stakishari wakamatwa na Polisi… Wamachinga wanaendelea na ujenzi wa vibanda Jangwani pamoja na Serikali kusisitiza kuwa wanapaswa kuhama eneo hilo. 

Wasanii waingia mitini kwenye kikao kilichoandaliwa na idara ya mawasiliano TCRA na kati ya wasanii 70 walioalikwa waliofika ni wasanii chini ya 20… Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti @CloudsFM nimekurekodia na kukuwekea hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.