Thursday, August 20, 2015

Anonymous

VIUMBE WA AJABU! MAREKANI WADAIWA KUWATUMIA KUVUMBUA TEKNOLOJIA MPYA - 3


Nakumbusha kuwa katika uumbaji Mungu, aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Wiki kadhaa niliona ni vyema tukajifunza vitu nje ya boksi. Ni juu ya uwepo wa viumbe wa ajabu waishio angani waitwao Aliens. Kwa muda mrefu viumbe hawa wamekuwa wakihusishwa na upotevu wa vitu na watu duniani.

Wiki iliyopita tuliishia pale tulipokuwa tunaangalia ukweli juu ya madai ya kuwepo kwa uhusiano kati ya wanasayansi wa Kimarekani na hawa Aliens, ikielezwa kuwa wamekuwa wakibadilishana teknolojia. Je, hilo linawezekana? ENDELEA NAYO…

Inaweza kukushtua kidogo lakini baadhi ya watu wanasadiki kwamba, inapotokea Aliens wakapata ajali angani, huwa Serikali ya Marekani inaagiza miili yao ifuatwe zaidi ya kilomita 1,448 kutoka Eneo la Area 51 lililopo Las Vegas, Marekani ili kuwatibu majeraha. Eneo hili, kama ilivyokuwa kwa Bermuda Triangle (nitakuletea simulizi yake kamili) nalo limekuwa maarufu mno kwa habari za Aliens na mauzauza yake.

Baadhi ya watu hudai Aliens wana maghala na stoo za teknolojia katika Eneo la Area 51, wakishirikiana kwa karibu na wataalam wa anga wa Marekani.Japo ni siri kubwa lakini inaaminika kuwa wapo Aliens wanaoishi eneo hilo. Maswali juu ya hilo ni mengi hasa njia ya mawasiliano wanayotumia na aina ya vyakula wanavyokula.

Katika eneo hilo mambo mengi ya kiteknolojia yamekuwa yakishuhudiwa na watu waishio jirani.
Kuna majengo ya ajabu ambayo ndani yake haijulikani kuna nini. Inaaminika hapo ndipo Aliens hubadilishana teknolojia na Wamarekani. Kivipi?

Wapo wanaoamini kuwa Aliens ndiyo huwaongoza wanasayansi hao hasa wanapokuwa kwenye jambo au jaribio la uvumbuzi wa teknolojia mpya.Inasemekana kuwa, kwa sasa wapo kwenye mpango wa kujaribu kutengeneza kiumbe chenye mchanganyiko wa binadamu na Aliens kwa sababu hawawezi kuzaliana na binadamu wa kawaida.

Pia wamekuwa wakihangaika kuvumbua teknolojia ya uwezekano wa binadamu kuwasiliana na ndugu au jamaa ambao walishafariki dunia.Kuna madai kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwekeza katika uvumbuzi huo huku binadamu wakitolewa wachinjwe bure ili kufanikisha jaribio hilo.

Wataalam wa anga wamekuwa wakikataa katakata kuwepo kwa uhusiano kati ya Aliens na Eneo la Area 51.
Pamoja na wataalam wa anga na marubani kukana habari hizo, lakini bado wananadharia wa kisasa wameendelea kujenga dhana kuwa Eneo la Area 51 lina uhusiano mkubwa na Aliens.

Mwaka 1987, jamaa aitwaye Robert Lazar aliituhumu serikali ya Marekani moja kwa moja kuwa ilikuwa ikishikilia Aliens tisa katika eneo hilo ambao walikuwa wakisaidia kupatikana kwa teknolojia ya kuboresha masuala ya kivita angani.

Kwa mujibu wa Lazar, aligundua uwepo wa mabaki ya vitu maalum alivyoviita Element 115 ambavyo vinafanana na hawa Aliens. Watu wengi waliamini madai ya Lazar ni ya uongo, lakini alipojitokeza kwenye televisheni mwanzoni mwa miaka ya 80 akifafanua mambo hayo, ndipo umma ukavutiwa na mawazo yake kuhusu hawa Aliens kwenye Eneo la Area 51.

Kwa miaka mingi sasa, serikali ya Marekani imekuwa ikilitumia eneo hilo kujaribia ndege zake hasa za kivita.
Itaendelea wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.