Thursday, August 20, 2015

Anonymous

MTUKUTU RIHANNA AKANUSHA KUTOKA NA STAA HUYU WA NBA



Diva wa R&B asiyekaukiwa vituko kutoka nchini Marekani, Robyn Rihanna Fenty ‘RiRi’.
New York, Marekani
DIVA wa R&B asiyekaukiwa vituko kutoka nchini Marekani, Robyn Rihanna Fenty ‘RiRi’ hivi karibuni amekuja juu baada ya staa wa NBA, Matt Barnes kudai kuwa kwa sasa wapo karibu na ikiwa mipango yao itakwenda vizuri, siku si nyingi wanaweza kudumbukia kwenye dimbwi la malavidavi kulifufua upya penzi lao.
Skendo hiyo ya Matt aliyewahi kutoka kimapenzi na RiRi huko nyuma, ilianza kusambazwa mapema wiki iliyopita na aliyekuwa mke wa mcheza basketi huyo, Gloria Govan akidai kuwa Matt na Rihanna kwa sasa ni wapenzi tena na mara kwa mara wamekuwa wakikutana sehemu tofauti ambazo si rahisi kwa watu ambao hawana uhusiano kukutana.

Kwa upande wake RiRi, baada ya kuzinyaka ‘drama’ hizo zilizokuwa zinaendelea kwenye mitandao ya kijamii alikanusha madai hayo kwa kutupia kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram kinachoonesha mahojiano kati ya Matt na kituo fulani cha habari kisha akaambatanisha maandishi yaliyokanusha madai hayo. “Shetani muongo, hakuna kinachoendelea kati yetu, hakuna lolote,” aliandikaRihanna.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.