Monday, August 10, 2015

Anonymous

VIDEO: Mtangazaji alivyovamiwa na kuuawa akiwa kwenye Kipindi redioni…

Hili ni tukio ambalo limechukua sana headlines mitandaoni na kwenye Vyombo vya Habari vikubwa vya Kimataifa Duniani, mtangazaji kavamiwa akiwa anarekodi show yake kwenye Kituo cha Radio Brazil !!
Kinachoibua maswali kwa upande mwingine ni kuhusu nani kahusika na mauaji hayo? wauaji waliingia mpaka ndani na kuua alafu wakafanikiwa kutoka salama, mtangazaji Gleydson Carvalho kauawa kwa kupigwa Risasi tatu kichwani na kifuani.
4221396001_4407550888001_Radio
Wauaji hao walivamia na kumzidi nguvu mtu wa mapokezi, wakamkamata producer wa show akalazimishwa kuingia chini ya meza… alafu wakamalizia kwa kumuua mtangazaji huyo ambaye alikuwa maarufu sana kutokana na kuikosoa Serikali kushindwa kupambana na tatizo la Rushwa.
Shuhudia video hiyo hapa....
‘Sikuwahi kufikiria kitu cha aina hii kitakuja kutokea ndani ya nchi yetu… hili ni tukio linalostahili Uchunguzi makini sana kufanywa na Serikali‘– amenukuliwa Marcos Coelho, Mwanasheria wa Mtangazaji huyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.