Monday, August 10, 2015

Anonymous

LOWASSA na NEC.. Lipumba kuondoka CUF? ni CCM ‘A’ na CCM ‘B’? Kimbisa kagoma CCM? >Stori Kubwa (Audio)

ioo
Uchambuzi wa magazeti redioni umekupita? Nimefanya jitihada ya kukusogezea zile zote kubwa kubwa zilizoweka vichwa vya habari kwenye magazeti August 10 2015 zikiwemo na hizi !!
Joto la uteuzi wa Ubunge CCM lazidi kupanda Dodoma… siri ya Prof. Ibrahim Lipumba kutoka CUF yafichuka, mipango ya Edward Lowassa yaivuruga CCM… CCM yabomoka zaidi, wanachama 100 wajiunga CUF. 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa asema CCM haitishwi na watu wanaohama Chama hicho na hakiwezi kuendeshwa kwa vitisho hivyo na kitaendelea kushika dola. 

Edward Lowassa kuchukua fomu ya kugombea Urais leo kwenye Makao Makuu ya NEC, asema wapinzani wakiikosa nchi mwaka huu watasubiri miaka 50 huku akiituhumu CCM kwa kuwa wadau wa kuiba kura. 

Prof. Ibrahim Lipumba aibukia Kigali asema UKAWA wamefanya Uchaguzi kuwa wa CCM ‘A’ dhidi ya CCM ‘B’... na Rais Jakaya Kikwete azindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio Mtwara.
Uchambuzi ulifanyika OnAIR @CloudsFM, niliurekodi na unaweza kusikiliza hapa stori zote mtu wa nguvu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.