Sunday, August 2, 2015

Anonymous

TETESI ZA USAJILI ULAYA: VAN GAAL AITAKA MAN UTD KUMUUZA DE GEA..PSG NA DI MARIA MAMBO SAFI...PEP GUARDIOLA KUTUA MANCHESTER

VAN GAAL AITAKA MAN UTD KUMUUZA DE GEA:

Meneja wa kilabu cha Manchester United Louis van Gaal kwa sasa anaitaka klabu hiyo kumuuza David De Gea kwa Real Madrid kwa kuwa mawazo ya golikipa huyo yameathiriwa na makubaliano kati ya vilabu hivyo.
Chanzo: AS
Jumamosi, 8/1/2015 09:46

MAN CITY WANAJIPANGA KUMNYAKA PEP KWA £100M:

Manchester City wanaamini kuwa watamnyaka kocha wa Bayern Pep Guardiola kwa dau la kushangaza la pauni milioni 100. Bosi huyo wa Bayern Munich, ambaye anaonekana kuwa tayari kuhama Ujerumani, anajipanga kuchukuwa nafasi ya Manuel Pellegrini msimu ujao kwa mkataba wa pauni 20 milioni kwa msimu.
Chanzo: The Sun
Jumamosi, 8/1/2015 00:02

DI MARIA AMEKUBALIANA VIGEZO NA PSG:

Angel Di Maria amepiga hatua karibu na kujiunga na PSG baada ya kukubaliana vigezo binafsi, huku Margentina huyo akitegemewa kukamilisha vipimo vya afya mapema wiki ijayo. Winga huyo atasaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya euro milioni 10.5 kwa msimu na bei ya uhamisho waliyokubaliana na Manchester United ni euro milioni 63.
Chanzo: TRMC
Ijumaa, 7/31/2015 21:54

INLER AITOLEA NJE LEICESTER:

Kiungo wa Napoli Gokhan Inler amekataa kuhamia Leicester City. Vilabu hivyo vimekubaliana ada ya euro milioni 4 (£2.8m).
Chanzo: Sky Sport Italia
Jumamosi, 8/1/2015 09:45

BERBATOV AFANYA MAZUNGUMZO NA ASTON VILLA:

Dimitar Berbatov atasafiri kuelekea Birmingham siku ya Jumatatu kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na bosi wa Aston Villa Tim Sherwood juu ya uhamisho uliopendekezwa. Villa wanataka kuongeza nguvu katika nyanja ya ushambuliaji na huenda dili hilo likakamilika ndani ya wiki.
Chanzo: Daily Express
Ijumaa, 7/31/2015 21:43

AKPOM KUJIUNGA NA HULL CITY KWA MKOPO:

Licha ya kusisitiza kuwa hatotolewa kwa mkopo, Arsene Wenger amekubali kumtoa kwa mkopo Chuba Akpom kwa kilabu cha Hull City kwa kampeni ya 2015-2016. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 licha ya kuonesha makali katika michezo ya maandalizi ya msimu anajipanga kushiriki Championship.
Chanzo: BBC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.