Sunday, August 2, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: MBOWE ATOA KAULI KUHUSU TETESI ZA DR SLAA KUJIUZULU!

Akizungumza na Radio one mda wa saa 4, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Dr Slaa hawezi kuhama chama hicho na hafikirii kamwe, kwa sasa anapumzika kwa likizo ya wiki moja.

Alipoulizwa kuhusu Slaa kutokubaliana na ujio Wa Lowassa amejibu kila kitu tulikubaliana na Slaa mwenyewe aliunga mkono suala hilo. 

Mbowe amesema wananchi na wanachadema kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwani hiki chama ni makini na hakiwezi fanya maamuzi bila maridhiano na akasisitiza kuwapuuza wanaoeneza habari kuwa Slaa amejiuzulu siasa.

Alipoulizwa mara ya mwisho kuwasiliana na Dr Slaa ni lini akajibu jana saa kumi na mbili jioni.
Alipoulizwa walizungumza nini akajibu anajua yeye na Slaa.
Walipomuuliza hasa mbona sisi tukimpigia hapatikani akajibu sijui lakini mimi nimewasiliana nae jana.

Chanzo: Radio one
Chanzo: Radio one

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.