City kupitia kwa mkurugenzi wake mtendaji Txiki Bergistan wanajiandaa kupeleka ofa ya euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo ambapo inaelezwa kuwa ofa yao inazidi ofa ya United kwa euro milioni 4 ambapo United wametoa ofa ya euro milioni 26.
United kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakitajwa kuwa karibu kumsajili mchezaji huyu ambaye ni dhahiri hana nafasi ya kuumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona na ameweka wazi azma yake ya kutaka kuondoka.
Manchester City wanaonekana kutumia faida ya ukaribu ulioko kati ya wakurugenzi wake wawili Txiki Bergistan na Feran Soriano na klabu ya Barcelona ambapo wawili hao waliwahi kufanya kufanya kazi kwa miaka mingi kwenye klabu hii ya huko Catalunya .
Hata hivyo bado ofay a Manchester City haijawasilishwa rasmi kwa Barcelona na hadi sasa mazungumzo rasmi ambayo yamefanyika ni kati ya Barca na United na inaweza kufikia hatua ya mchezaji mwenyewe kuchagua mahali anakotaka kwenda .

Note: Only a member of this blog may post a comment.