Tuesday, August 25, 2015

Anonymous

SIMBA SC kumtema Papa Niang? Hili ndio jina la msenegal mwingine anayekuja SIMBA SC

Klabu ya soka ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita ilimleta mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papa Niang ambaye ni ndugu wa damu na Mamadou Niang mchezaji aliyetamba katika vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo timu ya taifa ya Senegal.
DSC_9335
August 24 Papa Niang alijaribiwa na wekundu hao wa msimbazi katika mechi ya kirafiki ya Simba dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga inayofundishwa na kocha Jamhuri Kiwelo, taarifa zilizotoka ni  kuwa Niang hajafanya vizuri majaribio ya Simba hivyo August 25 inaleta msenegal mwingine kuja kumfanyia majaribio. 
Taarifa zinaeleza Simba inamleta Pape Abdoulah Nd’aw kutoka Senegal ila analetwa na wakala aliyemleta kocha wa Simba Dylan Kerr, msenegal huyo anayekuja Simba inadaiwa ameshawahi kucheza Ulaya katika klabu ya Bucharest ila alivunja mkataba baada ya kutolipwa fedha anazodai.
CHAZNO CHA HII STORI:SALEH JEMBE

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.