Friday, July 17, 2015

Anonymous

ALIYETOSWA URAIS CCM, AOMBA ASHIRIKI KAMPENI!

Aliyekuwa akigombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Amos Robart Siyantemi (kushoto) akisoma taarifa yake, pamoja na Ofisa Habali wa Idara Habari Maelezo, Pius Yalula.
...akionesha msisitizo wa Jambo.
Wanahabari wakichukua tukio.
MMOJA wa makada 37 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wakiwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya chama hicho, Amos Robart Siyantemi ameomba kujumuishwa katika kampeni za kumnadi John Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu

Katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Siyantemi alimuomba Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake Philip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana kumshirikisha katika timu ya kumnadi mgombea huyo, kwani hivyo ndivyo alivyowaahidi wananchi wakati akitangaza nia ya kuomba nafasi hiyo.

“Naiomba Kamati Kuu inishirikishe kwenye timu ya mgombea wetu, ninamwomba pia mgombea wetu John Pombe Magufuli afahamu kuwa kwa sababu ya ugumu wa itifaki katika kumuona, naomba anijumuishe katika timu ya kampeni. Hii yote ni kuonyesha kuwa ndani ya chama chetu bado kuna mshikamano mkubwa miongoni mwa wanachama.”
(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.